Skip to main content

Posts

Showing posts from October 23, 2015

WAHUKUMIWA JELA MMOJA KILA MOJA KWA KWA KUJIANDISHA MARA MBILI BVR

WAKATI wananchi wanajiandaa kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewahukumu Majuto Kisumbe (22)na Zawadi Mdegela (33) kulipa faini ya laki moja au kwenda jela mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura . Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema Kisumbe na Mdegela wamehukumiwa kulipa faini au kenda jela mwaka moja kwa kosa la kujiandisha mara mbili kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura (BVR) kinyume na Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010. Alisema kuwa katika nyakati tofauti Kisumbe, mkazi wa Mahenga wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa na Zawadi Mdegela wa Ifunda wilayani Iringa walijiandikisha mara mbili katika BVR katika vituo viwili tofauti.  Hakimu Mkazi Andrew Peter Scout alisema Kisumbe alitenda kosa hilo tarehe 04 Aprili mwaka huu katika Kijiji cha Mahenge, Wilaya ya Kilolo. Alisema kuwa mtuhumiwa Kisumbe al...

RIPOTI MAALUM: MABADILIKO YA TABIANCHI YAATHIRI VISIWA VYA MAFIA NCHINI TANZANIA

Moja ya eneo lililoaribika kutokana na hali ya mabadiliko ya tabianchi (Climate Change) katika fukwe ya Kilindoni, katika Kisiwa cha Mafia, Mkoani Pwani, nchini Tanzania. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog). Na Andrew Chale [MAFIA-ISLAND] Kisiwa cha Mafia kijografia kipo karibu na mlango wa Mto Rufiji kusini mwa Tanzania. Hata hivyo, Kisiwa hichi ambacho ni Wilaya moja wapo ya Mkoa wa Pwani inakabiriwa kwa kiwango kikubwa na changamoto za Mabadiliko ya tabianchi hasa baada ya wananchi wake wengi kutopata elimu hiyo sahihi. Imeelezwa kuwa, elimu juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika Kisiwa cha Mafia ambacho pia kinaunda visiwa vidogovidogo zaidi ya vitano, wananchi walio wengi katika kisiwa hicho bado hawajapata elimu sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya kimazingira (Climate Change). Mtandao huu ambao ulipiga hodi katika kisiwa hicho cha Mafia ili kupata habari za mabadiliko ya tabianchi na namna ya Mabadiliko ya tabianchi yanavyo at...