Skip to main content

Posts

Showing posts from June 4, 2017

Unywaji maziwa bado tatizo mkoani Iringa

Walimu wa shule ya Msingi JJ Mungai Manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wao baada ya kupewa mgao wa maziwa na Kampuni ya Asas Dairies Ltd ya mjini Iringa jana. Watanzania waliungana na wenzao katika kuadhimisha Wiki ya Unywaji Maziwa ambapo kilele cha maadhimisho kilikuwa juni mosi mwaka huu. Katika maadhimisho hayo, imebainika kuwa Watanzania bado wako nyuma katika unywaji wa maziwa ikilinganishwa na nchi nyingine kama vile Kenya. Meneja wa miradi wa Asas Group of Companies Ltd Hassan Swedi kwa upande amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kupenda kunywa maziwa kila siku badala ya kusubiri wang’atwe na nyoka au wadudu kutoa sumu mwiilini ama washauriwe na madaktari. alisema kuwa watu wengi wamekuwa wavivu katika suala la unywaji wa maziwa ikilinganishwa na kasi wanayoitumia kwenye unywaji wa pombe ambapo baadhi yao wamekuwa mabingwa wa kushinda au kukesha baa. Akaongeza kuwa viwango vinavyopendekezwa kimataif...

MAGAZETI YA LEO JUNE 4