Skip to main content

Posts

Showing posts from May 21, 2016

DC. BAGAMOYO AKABIDHI MADAWATI 50 KWA SHULE MBILI ZA MSINGI

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Hemed Mwanga,kulia mwenye miwani. akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya msingi Majengo madawati. Na Athumani Shomari,  Bagamoyo. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid HEmedi Mwanga amekabidhi madawati 50 kwa shule mbili za msingi ikiwa ni mkakati wa mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everisti Ndikilo wa kuondoa uhaba wa madawati unaozikabili shule za mkoa wa Pwani. Madawati hayo 50 yenye thamani ya shilingi milioni nne yamekabidhiwa kwa shule za msingi Majengo na Mbaruku zote za Bagamoyo mjini. Majidi amewashukuru wadau wa maendeleo ya elimu wilayani Bagamoyo ikiwemo kampuni ya Kirai Pateli ambayo ndiyo imetoa madawati hayo 50 ili kuondoa tatizo hilo kwa shule za serikali huku Shubashi Pateli amtoa ahadi ya kutengeneza madawati yote yanayohitajika kwa shule za Bagamoyo ambayo ni 1,353.  Ili kwenda sambamba na agizo la mkuu wa mkoa wa Pwani ambae amesema mpaka kufikia tarehe 30 may shule zote za mkoa wa Pwani ziondokane na uhab...