Skip to main content

Posts

Showing posts from August 30, 2011

UHABA WA MADAWATI LUGARAWA WANAFUNZI SABA WAKALIA DAWATI MOJA. FUNZA NI CHANGAMOTO KWA WATOTO HAO

      Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Lupefu, Lugarawa wakiwa darasani na Mwalimu Mary Mhagama huku wakiwa wamebanana saba kwenye dawati moja lenye uwezo wa watoto watatu. WANAFUNZI katika Shule ya Msingi ya Lupefu iliyoko Kata ya Lugarawa wilayani Ludewa, mkoani Iringa wako hatarini kukatika miguu na viungo vingine vya mwili kutokana na kuliwa na funza mikono na miguu yao kunakosabishwa na uhaba wa madawati ambapo sasa wanafunzi saba wanalazimika kukalia dawati moja. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Aprudensia Lugome amekiri kuwepo kwa matatizo hayo na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na ukata wa fedha unaoikabili shule yake pamoja na uelewa na mwamko mdogo wa wananchi juu ya elimu. Lugome alisema hulazimika kila wakati kununua pini madukani kwa fedha zake na kuwaita wazazi wa wanafunzi wenye mafunza kufika shuleni kushiriki kuwatoa funza watoto wao hata hivyo hufika wachache. ...

ZAHANATI YA KILONDO NA LIFUMA ZAPATA WAGANGA WASTAAFU NI BAADA YA MBUNGE KULIPA POSHO TOKA MFUKONI MWAKE

. WANANCHI katika Kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Iringa  wamepata furaha iliyopindukia na baadae kuikataa Boti iliyopelekwa na Mbunge wao   Deo Filikunjombe kama ‘Ambulance’ kwa ajili ya wagonjwa baada ya mbunge huyo kuwapelekea tena mganga katika zahanati yao. Kilio cha muda mrefu kwa Wananchi wa Kilondo ni mganga ndiyo maana mbunge wao alipowapelekea mganga na boti kwa wakati mmoja walichagua mganga na kusema hakuna haja ya boti kwa sababu waliomba boti ili kuwasafirisha wagonjwa kuwapeleka kwa mganga. Uamuzi wa mbunge huyo kuamua kutoa fedha yake ya mfukoni na kuwalipa posho waganga wastaafu ulikuja baada ya Halmashauri ya Wilaya kushindwa kupeleka waganga katika zahanati hizo huku wananchi wakipoteza maisha kwa magonjwa ya kawaida. Akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni Bw. Filikunjombe alisema kuwa wananchi wa Kilondo ni binadamu kam...

WANOVISI WAKIBENEDKTINI

Baadhi ya wanovisi kutoka mashirika mbalimbali ya kitawa na walezi wao wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Norbert Mtega (katika walioketi) katika kongamano lao la kubadilishana mawazo na ujuzi hivi karibuni. Walioudhuria kongamano hilo ni  watawa kutoka katika nyumba za kitawa za Peramiho (Wenyeji), Abasia ya Ndanda, Abasia ya Hanga, Abasia ya Mvimwa, Bikiria Maria Msaada wa Wakristo Ndanda-Ndolo, Mt. Agnes Chipole, Wakaimadores-Mafinga na Mt. Gertrude Imilwaha .