Skip to main content

Posts

Showing posts from October 28, 2017

DC MTATURU AZINDUA MSIMU WA KILIMO 2017/2018

Na Mathias Canal, Singida Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu amezindua msimu wa kilimo 2017/18 ikiwa ni Sehemu ya kuwasihi wananchi kuanza kujiandaa kwani tayari wakati wa kuanza kilimo umekaribia. Katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji na kata ya Ihanja wilayani Ikungi Mhe Mtaturu pamoja na mambo mengine lakini amewasihi kutumia vizuri mvua za mwanzo kupandia. Katika mkutano huo wa uzinduzi Mhe Mtaturu pia ameanzisha utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka ili kuwaandaa wakulima kuingia msimu mpya mapema ikiwemo kuyakumbusha makampuni ya mbegu kuwafikishia wakulima mbegu kabla mvua kuanza kunyesha. Sambamba na utaratibu huo wa kuzindua msimu wa kilimo kila mwaka pia kutakuwa na zoezi la kufanya maonesho ya zana na teknolojia mbalimbali za kilimo ili wakulima wapate muda wa kujifunza mbinu mpya za kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara. Mhe Mtaturu aliwaagiza maafisa ugani ...