Skip to main content

Posts

Showing posts from January 30, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI

Dkt. Kigwangalla awapa funzo watumishi wa sekta ya afya, awataka kuwa wabunifu

Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha sekta ya afya nchini, watumishi wa sekta ya afya wametakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu. Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa, Dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali, kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara, Felix Zelote akimpatia maelezo waziri huyo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akibadilishana mawazo na wataalamu wa hospitali hiyo kwenye chumba cha upasuaji Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akitembelea Hospitali ya Mount Meru iliyopo mkoani Arusha. Amesema hospitali zinatakiwa kusimama zenyewe kwa ukusanyaji wa mapato,hivyo upo ulazima wa kujenga au kukarabati majengo ambayo wanaweza kufanya wodi za kulipia ambazo zitakua zenye ubora ...

RAIS MAGUFULI AMUONGEZEA MUDA WA KUSTAAFU JENERALI MWAMUNYANGE

RAIS John Magufuli amemwongeza muda wa mwaka mmoja, Mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini,J enerali David Mwamunyange, ambaye alitakiwa kustaafu leo baada ya kutimiza umri kwa mujibu wa katiba na sheria. Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo. Akizungumza na waandishi wa habari,leo mapema kwenye Makao makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)yaliyopo Upanga jijini Dar es salaam,Jenerali Mwamunyange amesema leo alitakiwa kuungana na Brigedia wanne wa Jeshi ya ulinzi nchini pamoja na Meneja Jenerali wawili, ambapo wote kwa pamoja kwa pamoja wamestaa ndani ya Jeshi kwa mujibu wa sheria ya jeshi hilo. “Mimi mwenyewe ilikuwa nistaafu kazi leo , lakini Rais na Amri Jeshi mkuu ameamua kunibakiza katika utumishi jeshini kwa mwaka mmoja kuazia leo  hadi tarehe 31 Januari 2017,”amesema Jenerali Mwamunyange eneral Mwamunyage amesema sababu iliyomfanya Rais Magufuli kumwongezea mda huo,imetokana na Rais kutopata mtu sahihi wa kujaza nafasi hiyo aliyonayo tena. Hat...

WATUMISHI WA HOSPITAL YA SEKOUR TOURE, HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA NA CHUO CHA IFM WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI LA KILA MWEZI

Dkt.Magreth William Magambo ambae ni Daktari Bingwa wa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akitoa ufafanuzi juu ya Ushiriki wa Watumishi wa Hospitali hiyo la kushiriki Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016. Na: George Binagi Amesisitiza wananchi kuwa na desturi ya kufanya Usafi wa mara kwa mara (Kila Siku) katika mazingira yao ili kuepukana na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kipindupi huku akikumbusha zaidi pia wanajamii kuzingatia kanuni za usafi katika maeneo muhimu kama vile vyooni. Kunawa mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni. Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akizungumza wakati wa zoezi la usafi la kila mwisho wa mwezi lililofanyika hii leo Jijini Mwanza.  Anasema watoa huduma mbalimbali (Madaktari, Waalimu, Wafanyabiashara nk) katika jamii lazima wawe ...