Skip to main content

Posts

Showing posts from March 22, 2014

ATAKAYETUKANA MATUSI HADHARANI KUPIGWA FAINI ELFU HAMSINI

Na Friday Simbaya, Songea Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mlimani katika Kijiji cha Peramiho ‘B’ wilayani Songea, mkoani Ruvuma, Bonventura Mhagama kwa kushirikiana na katibu wake, Asante Mbawa amesema   mwananchi   atakeyetukana matusi hadharani atatozwa faini ya shilingi elfu hamsini. Alisema kuwa kumezuka tabia kwa baadhi ya watu kitongojini kwa makusudi wameamua kutoa matusi ya nguoni hadharani kwa kisingizio cha kulewa pombe. Mwenyekiti huyo alisema hayo jana wakati wa mkutano wa kitongoji, ambapo alisisitiza kwamba ni wakati wa kutumia sheria ndogondogo kukomesha tabia ya watu kutukana matusi baada ya kutofautiana kauli. “Ni lazima tuishi katika jamii inayozingatia maadili, mtu mzima unapoporomosha matusi hadharani unamfundisha ni nini mtoto?”   alihoji mwenyekiti huyo. Alisema kitendo hicho katika kitongoji hakitavumilika kwa sasa kwa sababu sheria ndogondogo zitatumika kumshitaki mtu yeyote atakayetukana mwenzake ili mradi kuwepo na ushahidi. Katika m...