Skip to main content

Posts

Showing posts from August 24, 2018

Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa Makampuni ya Bima ya nchi za Mashariki na kusini mwa Afrika

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa 41 wa umoja wa kikanda wa makampuni ya bima ya nchi za Mashariki na kusini mwa Afrika (OESAI) ukiwa na lengo la kuendeleza vipaumbele vya kukuza soko la bima. Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na kamishna wa bima wa mamlaka ya usimamizi wa shughuli za bima nchini (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware wakati akitoa taarifa ya mkutano huo amesema kuwa mkutano huo utaleta manufaa kwa taifa kutokana na kuwa na wageni zaidi ya 350 kutoka mataifa zaidi ya 30 yanayohudhuria mkutano huo. “Makampuni ya bima, wafanyabiashara na watoa huduma changamkiani fursa hizo haswa wale waliopo Kwenye jiji la Arusha ili msaidie katika kukuza uchumi wa taifa letu.” Amesema Saqware. Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Khamis Sulemani amesema kuwa uwepo wa mkutano huo hapa nchini utasaidia kutoa elimu na uzoefu kwa makampuni ya ndani kujua jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza Kwenye sekta hiyo. ...