Skip to main content

Posts

Showing posts from September 23, 2015

WHAT TO EXPECT:Fetal Movement During Pregnancy

    SEE ALL  147 COMMENTS Your baby's activity level — the kicks, rolls, and wiggles you can feel — will vary throughout your pregnancy. Here's what to expect when it comes to fetal movement. 1K shares TRENDING WITH MOMS Pregnancy Sleeping Positions During Pregnancy Family 6 Brands of Soft Cheese Recalled for Links to Illnesses and Death Pregnancy Business Leaders Stand Up to Congress for Paid Family Leave Feeling your baby twist, wriggle, punch, kick, and hiccup is simply one of pregnancy's biggest thrills (and it sure beats heartburn , puffy feet, an aching back, and some of the other hallmarks of these nine months). There may be no better proof that a brand-new — and impressively energetic — life is developing within you. But fetal movement during pregnancy can also drive a mom-to-be batty with questions and doubts: Is my baby kicking enough? Too much? Does my baby have four legs (becau...

FUNGA KAZI YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. POMBE MAGUFULI GEITA

Sehemu ya Wananchi waliohudhuria Mkutano wa Dkt- John Pombe Magufuli katika uwanja wa Kalangalala Geita, Jioni hii. ‪

LOWASSA AKIWA JIMBO LA MTAMA, AZOA WANACHAMA WA CCM KIBAO

AZIMA UTATA WA MAKAIDI Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa jana alimwomba mwenyekiti mwenza wa umoja huo, Dk Emmanuel Makaidi kujitoa kugombea ubunge katika Jimbo la Masasi na kumwachia mgombea wa CUF, Ismail Makombe baada ya kukataliwa na wananchi. Uamuzi huo ulifikiwa katika Uwanja wa Bomani mjini Masasi, baada ya Lowassa kuwasimamisha wagombea hao jukwaani kuwanadi, lakini akapata upinzani mkali kutoka kwa wananchi alipompa nafasi Dk Makaidi. Lakini kabla Makaidi hajasema chochote aliondoka katika mkutano huo na meza kuu ilijadiliana, ndipo mke wa Makaidi, Modesta aliposhauri waachwe wote wawili wachuane hoja ambayo ilikubaliwa na Lowassa ambaye alitangaza tena kuwa wagombea hao kila mmoja atapambana kivyake. Awali, Lowassa alipotoa uamuzi wa kumuomba Dk Makaidi amwachie kijana huyo, uwanja mzima ulilipuka kwa nderemo na vifijo huku wananchi wakinyoosha mikono juu kuonyesha kukub...

WAKULIMA WANAWAKE WAPIGWA MSASA UONGOZI WA MWANAMKE KATIKA KILIMO

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi (DED) Saada Malunde akifungua semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima jana mjini Mafinga. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Shirika la Land O' Lakes chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani (USAID) (Picha na Friday Simbaya) MALENGO YA SEMINA Washiriki kufahamu hali ya upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wakulima hasa wanawake.  Kuchambua changamoto zinazokabili utoaji wa huduma za ugani kwa wakulima wanawake.  Mapendekezo ya nini kifanyike ili kuboresha upatikanaji wa huduma za ugani kwa wakulima. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi (DED) Saada Malunde akifungua semina ya uongozi wa mwanamke katika kilimo, upatikanaji wa huduma za ugani na pembejeo za kilimo kwa wanawake wakulima jana mjini Mafinga. Washiriki wakiwa katika vikundi mbalimbali vya majadiliano wakati wa semi...

LOWASSA ATOA KAULI YAKE JUU YA UTAFITI WA TWAWEZA...!

Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, CUF 1%, ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%. Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo. Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter >>> ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata‘  (POSTED BY EDWARD MICHAEL ON 9:22 PM -TANZANIA CLASSIC)

DKT. MAGUFULI APIGA PUSH UP JUKWAANI, NI WAKATI AKINADI SERA NGARA

MGOMBEA kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, akipiga pus up jukwaani wakati akinadi sera kwenye mfululizo wa kampeni mkoani Kagera jana.

CCM NAO WAPINGA UTAFITI WA TWAWEZA

Siku moja baada ya taasisi ya Twaweza kutangaza ushindi mnono kwa mgombea Urais wa CCM, Dk John Pombe Magufuli dhidi ya Mgombea Urais wa Ukawa Edward Lowassa, Kada wa chama cha Mapinduzi Januari Makamba amepinga matokeo hayo akidai wamepunguziwa ushindi. Makamba amesema kwamba utafiti huo umewapunguzia ushindi chama cha Mapinduzi kwa kuwa katika utafiti wao ulionesha Magufuli angeshinda kwa asilimia 69 dhidi ya asilimia 65 ya Twaweza. Akizungumza na moja ya gazeti hapa nchini Makamba amesema CCM haistushwi na utafiti huo kwa mgombea wao amefika maeneo mengi nchini Tanzania kufanya mikutano. Akitangaza matokeo hayo mkurugenzi wa TWAWEZA Aidan Eyakuze, amesema utafiti huo ulifanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu, na ulifanyika kwa njia ya simu kukusanya maoni ya wananchi katika mikoa yote ya Tanzania. Eyakuze amesema kuwa wananchi waliulizwa swali kuwa watamchagua nani bila kutajiwa majina na walipoombwa kutaja moja kwa moja jina la mgombea Urais...

TASAF WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

Picha na Maktaba Wasimamiaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini mkoani Iringa wametakiwa kuimarisha uwazi, uwajibikaji na kuruhusu makundi tofauti kushiriki kwa kutumia mfumo madhubuti wa wanufaika. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya III iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Valentine mjini Iringa na kusomwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Seleman Mzee. Masenza alisema “ni mategemeo yangu kuwa utekelezaji wa mpango huu wa kunusuru kaya masikini utaimarisha uwazi, uwajibikaji na kutoa fursa kwa makundi mbalimbali kushiriki kwa kutumia mfumo madhubuti wa kubaini walengwa katika vijiji na mitaa yetu”.  Alisema muundo wa awamu ya tatu, umezingatia vema changamoto ambazo zilijitokeza katika utekelezaji wa awamu ya pili.  Alisema kwa maana hiyo usimamizi na ufuatiliaji umeimarishwa katika ngazi ya mkoa, halmasha...

UZINDUZI WA MSIMU MPYA WA TAMASHA LA MTIKISIKO IRINGA

RADIO Ebony Fm yenye makao yake makuu mkoani Iringa kupitia kipindi chake cha mchana "THE SPLASH" imezindua rasmi hewani (on air launching) msimu mwingine wa kila mwaka wa tamasha maarufu kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini linalokwenda kwa jina la "MTIKISIKO" ambalo linatarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu na kupita karibu sehemu zote inaposikika redio hiyo baadhi ya picha za watangazaji wakiwa katika shangwe za uzinduzi huo. (PICHA zote na Denis Mlowe)