Kamati ya Mfumo wa Ufuatiliaji wa Matumizi ya raslimali za Umma (PETS) Wilaya ya Iringa imetoa mapendekezo na maoni kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa kuhusu usimamizi endelevu wa pembejeo za kilimo ili kuongeza uwajibikaji, uwazi wa Jamii na viongozi. Kamati ya PETS Wilaya ya Iringa katika ziara yao waliyofanya katika kata za Kiwere, Maguliwa, Mgama, Ifunda na Wasa hivi karibuni walibaini changamoto mbalimbali na kutoa mapendekezo na maoni katika kuwainua wakulima wadogo wadogo kwa usimamizi endelevu wa pembejeo za kilimo ili kuongeza uwajibikaji, uwazi wa Jamii na viongozi katika Wilaya ya Iringa na Tanzania kwa ujumla. Katibu wa Kamati ya PETS wilaya ya Iringa kwenye kilimo, Hamida Tanda alisema jana kuwa Kamati ilibaini baadhi ya viongozi wa serikali, bado wana uelewa mdogo kwenye dhana ya ufuatiliaji wa raslimali za umma. Alisema kitendo cha wananchi kuhoji mapato na Matumizi kutoka kwa watoahuduma kinaonekana kuwa si jambo jema...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.