Skip to main content

Posts

Showing posts from February 4, 2018

DKT KIGWANGALLA ASITISHA VIBALI VYA KUHAULISHA MISITU YA HIFADHI ....

Waziri wa maliasli na utalii dkt hamisi kigwangalla akiongoza kamati ya misitu kutembelea msitu wa hifadhi wa Kihesa kilolo uliopo manispaa ya IRINGA kujiridhisha na mipaka kabla ya kuhaulisha sehemu ya msitu huo wenye ukubwa wa zaidi akari 500 kwa ajili shughuli za utalii jana. (Picha na Friday Simbaya) WAZIRI wa maliasili na utalii Dk.Hamis Kigwangala amewaagiza wakuu wa mikoa kote nchini kwamba wasihangaike kuandika barua za kuomba kuhaulisha misitu ya vijiji au halmashauri ili zitumika kwa shughuli za maendeleo. “Mimi hapa, nina msimamo mkali sana,Naomba Taifa lifahamu, lijuwe na viongozi wote wafahamu wasithubutu kuleta maombi ya kuhaulisha misitu iliyohifadhiwa kwa sababu hayo maombi nimekwisha yakataa kabla hayajafika mezani kwangu.”amesema Dk. Kigwangala na kuongeza:  “Kwa kipindi ambacho nitakuwa waziri wa mali asili na utalii sitohaulisha misitu hivyo viongozi wasahau kupoteza muda wao kuomba maeneo yaliyohifadhiwa kwamba yahaulishwe kwa ajili ...