Skip to main content

Posts

Showing posts from August 17, 2015

DJ WA KINAIJERIA KUFANYA ONYESHO NA KUTOA MSAADA KWA JAMII JIJINI DAR ES SALAAM

Mtengenezaji wa muziki, mtunzi wa nyimbo na DJ raia wa  Naijeria anayefanya kazi zake nchini Marekani Bi. Florence Ifeoluwa maarufu kama DJ Cuppy akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Slipway jijini Dar Waandishi wa habari wakiwa kazini

WAZAZI MATINEJA WAHITIMU ELIMU MBADALA

Second Secretary wa Ubalozi wa Japan, Noriko TANAKA (kulia) akipokea kitabu cha wageni kutoka kwa Mratibu wa kata ya Segese iliyopo halmashauri ya Msalala, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, Bi. Victoria Maige alipofikia katika ofisi hizo kwa ajili ya zoezi la kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye mahafali ya Mpango wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO. Na Mwandishi Wetu, Shinyanga WAZAZI wenye umri mdogo 149 mkoani Shinyanga ambao walipata mimba wakiwa shuleni wamekamilisha mafunzo ya miaka miwili ya stadi mbalimbali za maisha mkoani hapa. Wazazi hao wenye umri mdogo ni miongoni mwa wazazi 220 walioanza mafunzo hayo miaka miwili iliyopita chini ya mradi wa Elimu Mbadala kwa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhiliwa na Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO. Wazazi hao vijana kutoka wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga za halmashauri ya Shinyanga,...