LEAT IMEANZA MCHAKATO WA KUZIWEZESHA SERIKALI ZA VIJIJI KUANDAA SHERIA NDOGO ZA USIMAMIZI WA MALIASILI NA MAZINGIRA
Katika kufikia malengo ya mradi wa ‘Ushiriki wa Wananchi katika Usimamizi wa Maliasili, unaotekelezwa mkoani Iringa; Timu ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) imeanza mchakato wa kuziwezesha serikali za vijiji kuandaa sheria ndogo zitakazo waongoza katika usimamizi wa maliasili na mazingira. Sheria hizo zitasaidia kupunguza uharibifu wa rasilimali misitu na wanyamapori ambazo zipo katika hatari ya kutoweka kutokana na uvunaji haramu. Kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi katika wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa; LEAT ilifanya utafiti juu ya kiwango cha ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa maliasili, pamoja na mambo mengine katika utafiti huo LEAT ilibaini kuwa baadhi ya vijiji havikuwa na sheria ndogo ambazo zingetumika kusimamia maliasili na mazingira. Kutokana na hali hiyo LEAT imeanza mchakato wa kuziwezesha serikali za vijiji kuandaa sheria hizo. Vijiji vitakavyo wezeshwa katika awamu ya kwanza ni vijiji vya Mbweleli, Kinyika...