Skip to main content

Posts

Showing posts from January 27, 2026

Zaidi ya Wananchi 500 Wanatarajiwa Kupata Huduma za Macho na Meno Songwe

Songwe. Zaidi ya wananchi 500 wanatarajiwa kufikiwa na huduma za matibabu ya macho pamoja na afya ya kinywa na meno kupitia kambi maalum ya matibabu ya siku tano iliyoanzishwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Juma Ramadhani , amesema kambi hiyo imelenga kuwahudumia wananchi, hususan wanaoishi maeneo ya vijijini, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya umbali, gharama kubwa za matibabu pamoja na uhaba wa wataalamu wa afya ya kibingwa. Akizungumza na The Citizen leo Januari 27, 2026, Dk Ramadhani amesema katika kipindi cha siku tano, hospitali inatoa huduma za uchunguzi wa macho, matibabu ya magonjwa mbalimbali ya macho, ushauri wa kitaalamu pamoja na huduma za uchunguzi na matibabu ya kinywa na meno kwa gharama nafuu au bure, kulingana na hali ya mgonjwa. “Tumeona ongezeko la magonjwa ya macho na matatizo ya meno katika jamii, hivyo tumeamu...