Haya ni maneno ya Jackline Masisa (17), aliyekatiza masomo akiwa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mondo wilayani Kishapu, baada ya kupewa mimba na mwalimu wa shule jirani na mahali alikokuwa anapata huduma ya masomo ya ziada au tuisheni. “Akimaliza kunifundisha, alikuwa ananishikashika na kunivua nguo, kisha kunilaza…” anaendelea kusimulia Jackline, akimueleza mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 30 (jina linahifadhiwa). Anasema mwalimu huyo alimshawishi kuingia katika masomo ya ziada, yaani tuisheni, lakini baada ya muda wakageukia mapenzi. Jackline anakiri alizamishwa katika mapenzi na mwalimu wake kwa ushawishi wa ‘posho’ ya Sh. 5000 na matokeo yake, hivi sasa ana mtoto mwenye miaka miwili analelewa na wazazi wake, baada ya mwalimu aliyempa mimba kumkana. Ilikuwaje baada ya wazazi kugundua yu mja mzito? Kwanza anaanza kusema namna alivyoingia katika maisha mapya ya ujauzito. Bila ya kujitambua ana hali gani wakati huo , Jackline anasimulia, huk...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.