Skip to main content

Posts

Showing posts from August 5, 2016

RC MWANZA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa. Na BMG Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo. Akifungua rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda ya ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho yatakapomalizika. Alisema mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya mikoa hiyo kuwa ...