Skip to main content

Posts

Showing posts from February 23, 2017
Zoezi la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani linalofanyika kwa siku tangu kuanzia jana, linaendelea katika viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela. Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) amebainisha kwamba jana zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70 walihudumiwa na kurejea nyumba. Alisema zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari, presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada wanaosaidizana na wataalamu wazawa. #BMGHabari Umati wa akina mama waliojitokeza kwenye zoezi la upimaji afya bure katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya Zoezi la kuchukua taarifa likiendelea kwa umakini Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana na linasimamiwa na wataalamu wa afya k...

KAIMU MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA TAYODEA KWA KUSAIDIA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akibadhi vifaa vya vijana wa mradi wa WEKEZA (Wezesha Ustawi Endelevu kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa watoto) kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyegea na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim  Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyege akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza. Mwenyekiti wa Tayodea Stephen Kiama Mwaimu akizungumza wakati wa halfa hiyo  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza akizungumza kwenye halfa hiyo  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa baadhi ya vifaa vya ushonaji waliokabidhiwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kush...