Skip to main content

Posts

Showing posts from September 16, 2010

MAMBO YA LIVYOKUWA KATIKA UZINDUZI WA DARAJA LA MOJA

Wakati wa jua kali na uchovu wa kazi baada ya uzinduzi wa Daraja la umoja linaloziunganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji, Mtangazaji Maarufu wa TBC Taifa (zamani RTD), Bw. Malima Ndelema akipooza uso kwa maji ya Mto Ruvuma katika eneo la Mtambaswala upande wa Msumbiji hivi karibuni. Daraja la Umoja linalounganisha nchi mbili za Tanzania na Msumbiji lenye urefu wa kilometa moja kasoro katika Mto Ruvuma eneo la Mtambaswala ni kivutio cha kipekee katika masuala mazima ya utalii na kukuza ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.  Ubovu wa miundombinu ya barabara katika maeneo mengi ya vijijini na mijini yanakwamisha maendeleo ya wananchi na nchi yao kiuchumi, eneo hili kama linavyoonekana mbele ya Mto Rufiji eneo la Nangulukulu  Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ni kikwazo kikubwa cha wasafiri wa maeneo ya Kusini mwa Tanzania hasa wakati wa mvua. Msururu wa magari haya ni kielelezo tosha cha hali hiyo .

MTEMVU AWAONDOLEA WASIWASI WANANCHI

Abasi Mtemvu akiwapungia mkono wananchi wa Kata ya Azimio Jimbo la Temeke wakati akiwasili kwenye mkutano wa kampeni za uchguzi jimboni humo jana. MGOMBEA kiti cha Ubunge Jimbo la Temeke kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abasi Zuberi Mtemvu amewatoa wasiwasi wapangaji wa nyumba za kota zilizopo Temeke mwisho kwa kuwaeleza kuwa zoezi la kuvunjwa kwa nyumba hizo sasa limesitishwa. Mgombea huyo alitoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi uliyofanyika katika uwanja wa MjiMpya Kata ya Azimio jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na umati wa watu. Akifafanua zaidi kuhusu kauli yake hiyo Mtemvu alisema serikali iliyoko madarakani imejipanga kujenga majengo ya ghorofa katika eneo hilo ambapo ujenzi wake ukikamilika wapangaji wa awali wa kota watapewa umuhimu wa kwanza kufikiriwa katika kupanga kwenye maghorofa hayo. Alisema si vyema kuanza zoezi la uvunjaji wa kota hizo bila kuzingatia usalama wa wananchi na mali zao katika kipindi cha mpango huo. ...