Skip to main content

Posts

Showing posts from November 15, 2016

SERIKALI KUBORESHA MITAMBO YA KUCHAPISHA NYARAKA YA KIWANDA CHA UHAMIAJI KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata huduma Makao Makuu ya Idaya ya Uhamiaji wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya leo Kurasini jijini Dar es Salaam. Waziri Mwigulu akiwasili kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba za makamishna wa Uhamiaji zinazojengwa Kijichi jijini Dar es Salaam kuzikagua.  Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Abbas Rovya (kushoto), akimpigia saluti Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) kabla ya kukagua nyumba hizo za kisasa. Kulia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji (DCI), Shaban Hamza. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia), akiangalia nyaraka mbalimbali zinazochapishwa katika kiwanda cha kuchapa nyaraka za Uhamiaji alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kijichi jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji (ASP), Singwa Mokiwa na Kaimu Kamishna Generali wa Uhamiaji, Victoria Le...

SERIKALI KUJENGA VITUO VITATU KWA KILA HALMASHAURI KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI NA MLANGO WA KIZAZI

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza hii leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Bure ya Uchunguzi na Matibabu ya Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi mkoani Mwanza. Amesema serikali itaendelea kuboresha huduma za saratani ikiwemo kupatikana katika hospitali za rufaa Bugando Jijini Mwanza na KCMC Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam. Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema watanzania wengi wanakabiliwa na magonjwa ya saratani na kuwahimiza kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara. Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye ufunguzi huo Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, akizungumza kwenye uzinduzi huo, ambapo amesema uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi uliofanyika katika halmashauri za Buchosa, Ukerewe na Kwimba umewafikia wanawa...

WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI WAANZA MITAHANI YAO LEO

NA KAROLI VINSENT Jumla ya wanafunzi 435,221wa kidato cha pili nchi nzima leo wametarajia kuanza mitihani yao ya taifa ya kidato cha pili. Ambapo kati yao wavulana ni 214,013 sawa na asilimia 49.17 na wasichana 221,208 sawa na asilimia 50.83. Mbali na hao wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao watahiniwa wasioona ni 67 na watahiniwa wenye uoni hafifu ni 306 ambao watapewa maandishi ya karatasi hukuzwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Katibu mkuu wa Baraza la Mitihani nchini,Dkt Charles Msonde amesema mtihani huo ambao umeanza mapema hii leo ambao unatarajia kumalizika Nombemba 25 ya mwaka huu. Amesema mtihani huo unalengo la kuwapima uwezo na uelewa kwa wanafunzi katika yote wajifunzayo kwa miaka miwili ya masomo yao huku wanafunzi wanaofeli wanakosa nafasi ya kuendelea na kidato cha tatu. Dkt Msonde amesema maandalizi yote ya mtihani huo yamekamilika ikiwemo kusambazwa kwa mitihani itakayotumika katika upimaji huo pamoja na n...

WAIDAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO WAPEWA SIKU 90,SOMA HAPO KUJUA

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa hadi sasa kuna jumla ya wadaiwa sugu 142,470 wenye mikopo ya shilingi 239,353,750,170.27 iliyokwishaiva hawajajitokeza wala kuanza kulipa mikopo yao. Akitolea ufafanuzi wa maana ya neo "Wadaiwa Sugu", Badru amesema kuwa ni wanufaika waliokopeshwa, muda wa matarajio ukapita bila kuwasilisha taarifa zao na kulipa madeni ya mikopo waliyokopeshwa tangu mwaka wa masomo 1994/1995. Kuhusu hatua zinazochukuliwa na bodi hiyo, Badru amesema mbali na kutoa siku 30, bodi hiyo inakamilisha taratibu za kuwafikisha mahakamani kwa kuvunja sheria ya bodi ya mikopo kifungu cha 19A(1). Hatua nyingine ni pamoja na kuyawasilisha majina hayo katika taasisi za mikopo, kuwasiliana na wadhamini wao pamoja na kuyatangaza hadharani majina ya wadaiwa sugu wote ili waajiri, wadhamini na wadau wengine wayajue na kutoa taarifa katika bodi hiyo. Kuhus...