Na Friday Simbaya, Songea WAUMINI wa dini za kikristo katika mji mdogo wa Peramiho wamesherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo kwa kupata watoto 10 waliozaliwa siku ya mkesha mwaka huu, ukilinganisha na mwaka jana ambapo walizaliwa watoto saba katika hospitali hii, wakiume wakiwa watatu na wakike wanne, ikiwa ni ongezeko la watoto watatu zaidi. Kwa mujibu wa muuguzi wa zamu katika hospitali ya Misheni ya Mtakatifu Josefu Peramiho (St. Joseph Mission Hospital Peramiho) iliyopo Wilaya ya Songea vijijini, mkoani Ruvuma, Sista Matilda Mkulu alisema, kati ya watoto hao nane ni wa wakike na wawili wa kiume. Sista Mkulu alisema wote watoto kumi walizaliwa kwa njia ya kawaida na hakuna mtoto hata mmoja aliyezaliwa kwa operesheni. “Watoto wote walizaliwa kwa njia ya kawaida na hakuna mtoto aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri pamoja na mama zao. Katika kipindi hiki cha sikukuu ya krismas tumeamua kutoa zawadi ya sabuni za kufulia nguo za wat...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.