Skip to main content

Posts

Showing posts from October 4, 2017

AMKA NA MAGAZETI NA TUMBUSI BLOG

MCB YAUNGANA NA WATEJA WAKE KUADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DUNIANI

Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole,(kulia), akimpatia zawadi, mmoja wa wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Oktoba 4, 2017, kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam. Wiki ya kwanza ya Mwezi Oktoba kila mwaka, hutumika kama Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, ambapo taasisi za umma na binafsi, hujumuika pamoja na wateja wao kwa lengo la kuonyesha mahusiano mema katika kutoa huduma na pia kuzunhumzia changamoto za kihuduma kwa mwaka mzima na hatimaye kutafuta njia za kuzitatua changamoto hizo. Kwa upane wake, MCB iliwaalika wateja wake, na kujumuika nao kwenye tawi la benki hiyo, barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia wasaa huo kuwashukuru, wateja lakini pia kuwahamasisha zaidi kutumia huduma za benki hiyo ambazo ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la...