Na Friday Simbaya, Ludewa IKIWA imebaki siku moja tu kuanza kwa mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne nchini mwanafunzi Hosana Raaban wa Shule ya Sekondari Ulayasi Ludewa mkoani Iringa ametimuliwa shule baada ya kukamatwa na walimu wake akifanya mapenzi na mwanaume vichakani kinyume na sheria za shule. Mwanafunzi Hosana Raaban (20) anayetoka katika Kijiji cha Ligumbilo katika Kata ya Mlangali alikutwa na mkasa huo Oktoba 2 mwaka huu katika vichaka vinavyoizunguka shule hiyo baada ya kuwatoroka walimu waliokuwa wakisubiri kwa vifaa vya mitihani shuleni hapo tayari kwa mtihani kesho yake. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw Richard Chitundu akizungumza kwa njia ya simu alikiri kutokea kwa fumanizi hilo vichakani majira ya saa kumi na moja jioni na kukiri kosa na kutakiwa kufika kesho yake akiwa ama na mzazi au mlezi wake ili kupata ufumbuzi wa suala hilo, lakini mwanafunzi na wazazi wamekaidi agizo hilo. Akielezea tukio lenyewe Bw Chitundu...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.