Skip to main content

Posts

Showing posts from July 6, 2017

KINA DADA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI UVCCM

Katibu wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Iringa (UVCCM) James Mgego (pichani) amewahimiza vijana wa jumuiya hiyo kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hasa wa kina dada ambao wako nyuma kuchangamkia fursa hizo. Akoingea na SIMBAYABLOG jana katibu huyo alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi hilo ngazi ya mkoa ni vijana 44 tu kati yao wakina dada ni wanne, ikizingatia kuwa mwaka 2017 wa uchaguzi ndani CCM. Mgego alisema kuwa jumuiya hiyo ni jumuiya ya vijana ya CCM ni kwa ajili ya vijana wote wakiume na wakike lakini inashangaza kuona dada zetu wanakuwa nyuma kuchangamkia fursa za kugombea nafasi za uomgozi ndani ya umoja huo. Pia katibu huyo aliwataka vijana kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na kutowasikiliza watu ambao wapo kuona CCM inakwama katika uchaguzi huo wa ndani ya chama. Alisema kuwa zoezi la utoaji fomu za uongozi wa UVCCM ngazi ya mkoa ilianza tarehe 02.07.2017 na kukamilika tarehe 10.0...