Skip to main content

Posts

Showing posts from July 16, 2015

MWANAHABARI FRANK KIBIKI ACHUKUA RASMI FOMU YA UBUNGE LEO

MWANAHABARI Frank Kibiki achukua rasmi fomu ya kuomba ateuliwe kuwania ubunge wa jimbo la Iringa mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), leo.

MAKUSANYO YA MAPATO WILAYA YA MUFINDI YAONGEZEKA

Na Friday Simbaya, Mufindi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mufindi, Saada Malunde amesema makusanyo ya mapato yameongezeka kutoka zaidi ya shilingi bilioni 2,192,830,130/- mwaka 2010/2011 na kufikia zaidi ya shilingi bilioni 4,146,583,199/- mwaka 2014/2015. Mkurugenzi Mtendaji huyo alitoa taarifa hiyo hivi karibuni baada ya kuvunjwa rasmi Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi lililodumu kwa muda wa miaka mitano na kuoanisha mafanikio kadhaa yaliyofikiwa tangu kuundwa kwake mnamo mwaka 2010.

MUFINDI DISTRICT REVENUE RISES

THE Mufindi District Executive Director (DED), Saada Malunde said revenue has significantly increased from over 2,192,830,130/- billion in 2010/2011 to over 4,146,583,199/- billion in 2014/2015. The DED of Mufindi District Council (MDC) has issued the statement soon after the dissolution of the House of Councillors officially, which lasted for five years and mentioned several successful harmonizations achieved since its creation in 2010.   Malunde was presenting reports of the success of her district council during the dissolution of the Mufindi Full Council (Baraza la Madiwani), and cited some of these achievements that have included the establishment of the Mafinga Town Council (MTC) and also the increased revenue collection from more than 2,192 830,130 / - billion in 2010/2011 to reach more than a billion shillings 4,146,583,199/ - in 2014/2015. She said that the goal of the district council in secondary schools was to ensure all students entering secondary education ...

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Yahaya Msigwa ajitosa ubunge Iringa mjini

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Yahaya Msigwa akitoa ada ya shilingi laki moja kwa ajili ya fomu ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCM katika Jimbo la Iringa Mjini. (Picha na Friday Simbaya) Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Yahaya Msigwa akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCM katika Jimbo la Iringa Mjini. (Picha na Friday Simbaya) Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Yahaya Msigwa akiongea na wanachama kwa kuwaelezea nia yake ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCM katika Jimbo la Iringa Mjini katika Ukumbi Highland. (Picha na Friday Simbaya) Mwanachama mmoja Mary Kowi akimuuliza swali Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk. Yahaya Msigwa kwamba endapo atabahatika kuteuliwa na chama kupeperusha bendera na kushinda  ubunge kupitia tiketi ya CCM katika Jimbo la Iringa Mjini katika  uchaguzi mkuu mwaka huu, atawafanyia nini watoto yatima na wajane. Dk. Msigwa ametia nia na kuchukua fomu leo.(Picha na Friday...

MAMBO MATANO YALIYOMPA KIJITI MAGUFULI

Watanzania wengi na hata wagombea wa CCM walipigwa na butwaa kubwa baada ya kuona Dk John Magufuli anachaguliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. Ni watu wachache walimshtukia Dk Magufuli tangu awali na kuona uwezekano wa kiongozi huyo kufika happ alipo leo. Nataka tujadili mambo matano ambayo nayaona kama sababu za CCM kumpa kijiti “Tingatinga” huyu. 1. Kura za kanda ya ziwa Hili ni jambo la kwanza ambalo liliwafanya wapanga mikakati wa CCM kumvusha Magufuli. Ukiachilia mbali kufahamika kwake nchi nzima, lakini Magufuli anatoka kanda ya ziwa ambako kuna wapigakura wengi lakini kukiwa na ‘hatihati’ ya majimbo mengi kuelekea upinzani. Kanda ya ziwa si salama kwa CCM na lazima chama hicho kingehitaji mkakati wa kudhibiti wapigakura kwa kuwaletea kitu kitakachowaamshia matumaini mapya. Kanda ya ziwa inaundwa na mikoa ya Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Kagera, Mwanza, Geita na Mara na kuna jumla ya wakazi 11,832,857 kwa mujibu wa Sens...