Na Alex Mapunda, Ruvuma MWAKILISHI wa Kata ya Peramiho katika Mashindano ya Ansgar Cup ngazi ya Tarafa, timu ya Afya Fc imefanikiwa kuitandika bila huruma Kilagano Fc timu toka Kata ya Kilagano kwa kichapo cha bao 3-0. Katika mchezo huo ambao Mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Simon Bulenganija, bao la kwanza la Afya Fc liliwekwa kimiani na mshambuliaji machachari Emanuel Kajana dakika ya 39 ambalo liliwachanganya wachezaji wa Kilagano FC na wakaanza kucheza kwa Tahadhari kubwa. Dakika 15 za kipindi cha pili Kilagano Fc walicheza vizuri mno na walifanikiwa kufanya mashambulizi ya mara kwa mara katika lango la Afya Fc, lakini mambo yalikuwa tofauti baada ya mchezaji wa Afya Fc Shabiru Kinunga kuipatia timu yake hiyo bao la pili lililopeleka majonzi kwa Kilagano Fc mnamo dakika ya 60 ya mchezo. Lakini Kabla ya mpira kumalizika mfungaji wa bao la kwanza Emanuel Kajana alishindilia msumari wa moto katika vidonda vya Kilagano Fc...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.