Wengi sasa wafanyia biashara mtaani na majumbani. WAKATI Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ikilalamikia ufinyu wa Bajeti na kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo na huduma muhimu za jamii kwa kukosa raslimali fedha, wafanyabiashara katika soko kuu la mjini hapa wamelikimbia soko na kuamua kufanyia majumbani bila kulipa ushuru kutokana na soko hilo kukosa huduma muhimu za kiutu kama vile choo safi, maji na mlinzi. Wakizungumza katika soko jipya wafanyabiashara wa mbogamboga, nyanya, vitunguu na matunda walisema wanalazimika kukimbilia majumbani kwao hata kama ni mbali kwa ajili ya kwenda kujisaidia kutoka na soko hilo kuwa na vyoo vichafu vya zamani huku soko jipya nalo likikosa maji wakati vyoo ni vya kuflashi. ”Ndugu mwandishi hebu angalia na uingie wewe mwenyewe ndani ya vyoo hivyo kama unaweza kujisaidia na kuvumilia hali ya uchafu kila siku tunalazimika kwenda majumbani kujisaidia na kisha kurudi kuendelea na biashara.ni hatari sana inasikitisha,” alisema mmoja wa wafanyabiashara ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.