Skip to main content

Posts

Showing posts from October 21, 2017

SAUTI YA TUNDU LISSU YAMTOA MACHOZI HADHARANI ASKOFU HUYU ...

Moshi. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesimulia alivyobubujikwa machozi baada ya kusikia sauti ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu. Dk Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, amesema hayo baada ya Jumatano Oktoba 18,2017 Lissu kutoa salamu akiwashukuru Watanzania kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii. Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7,2017 mjini Dodoma. Soma: Lissu: Mungu alisema huyu hatakufa Sauti ya Lissu katika video hiyo ilikuwa ni ya kwanza kusikika tangu apelekwe jijini Nairobi Septemba 7. Alisikika akiwashukuru madaktari wa Nairobi na Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa kuokoa maisha yake. Pia, amewashukuru viongozi wa dini na wananchi kwa kumuombea, na taasisi za kitaaluma ndani na nje ya nchi ikiwemo TLS ambazo zilionyesha mshikamano mkubwa. Akizungumza...

Job Ndugai kuondolewa Bungeni ?

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa katika Bunge ambalo linatarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 anakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge, Job Ndugai Msigwa amesema hayo leo kupitia moja ya mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge atapeleka hoja yake hiyo ya kumuondoa Spika wa Bungue. "Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba" alisema Msigwa Mbunge Peter Msigwa ni kati ya wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akiendesha bunge kwa shinikizo na upendeleo na kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti hicho. Source: EATV

KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO...

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima.  WAKATI ikiwa imebakia mwezi mmoja tu kuelekea kwenye uchaguzi mdogo wa marudio wa udiwani kufanyika kutokana na kata mbali mbali kuwa wazi,TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), imesema hati ya kiapo cha mahakama ya kudhibitisha majina ya mtu(Affidavit), haitatumika katika kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa kata 43. Hati za kupigia kura zitakazotumika katika uchaguzi huo ni leseni ya udereva, Kitambulisho cha Utaifa na hati ya kusafiria. Hayo yamebainishwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima akizungumza na TUMBUSI BLOG na kwamba matumizi ya hati hizoyatapunguza biashara ya watu kununua au wizi wa vitambulisho vya kupigia kura na kuongeza uwanda mpana wa mtu kupiga kura.  "Hati ya kiapo cha mahakama cha kuthibitisha majina yako na taarifa zako haitaruhusiwa kupigia kura katika uchaguzi huu mdogo, kuna hati tatu tu ambazo zitaruhusiwa kutumika,"amesema. Kailima amesema hati ma...

Miaka 100 ya Skauti: Mkuu wa wilaya Sophia Mjema atoa agizo la uanzishwaji wa klabu za skauti kila...

Mkuu wa wilaya akizindua mapango wa mawasiliano kwa njia ya redio maalumu njia ya upepo na inteneti kwa skauti ‘Jamboree on the Air (JOTA), Mkuu wa wilaya ya ilala Sophia Mjema Akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wilaya ya ilala. Na Michael Utouh Mkuu wa wilaya ya Ilala ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake na wanafunzi wanaopata mafunzo maalumu ya scout alipofika kwa ajili ya kufunga makambi yao ya mafunzo siku ya leo. Mkuu wa wilaya akiwahutubia wanafunzi wa scout. Mmoja wa wakilishi wanafunzi wanaopata mafunzo ya scout wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi. Mkuu wa wilaya akikapewa maelekezo juu ya mpango anzilishi wenye lengo la kumkomboa mwana scout na baadhi ya mambo mengi kama vile Elimu nk. Akitembezwa pamoja na kukagua baadhi ya makambi ambayo wameyaweka wanafunzi...