Skip to main content

Posts

Showing posts from April 4, 2016

KLSA ASSOCIATES YAJIUNGA NA PKF, PROF. ASSAD AWATAKA KUONYESHA UBORA ZAIDI

Mgeni rasmi katika halfa ya uzinduzi wa ofisi za PKF Associates, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad akiwasili ukumbini na kukabidhiwa zawadi. (Picha na Rabi Hume wa Modewjiblog ) Katika kuhakikisha wanajitanua katika utoaji wa huduma bora za uhakiki na ukaguzi wa hesabu, kampuni ya KLSA Associates ya nchini imejiunga na mtandao wa kimataifa wa makampuni ya hesabu za kifedha na ushauri ya PKF ambapo baada ya kujiunga imebadilika jina kutoka KLSA Associates na kuwa PKF Associates Tanzania. Akizungumza katika halfa ya KLSA kujiunga PKF, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad aliwapongeza KLSA kujiunga na PKF na kuwataka kuongeza juhudi na kuboresha huduma zaidi kwa kuzingatia kwa sasa wamejiunga na kampuni ambayo inasifika duniani katika ukaguzi wa hesabu, utunzaji wa hesabu za kifedha, ufumbuzi na ushauri wa masuala ya kodi na kibiashara. “Tunafahamu jinsi PKF wanavyofanya kazi, mmepata nafasi ya ...

MDUARA UNAPOCHANGANYWA NA RAGGA JIBU NI "KITIMTIM" (VIDEO)

Muziki unakua sana na hivi karibuni wasanii wengi wa hapa nchini wamekuwa wakibuni mitindo ya aina mbalimbali ili kuzifanya kazi zao ziende mbali na kuvuta mashabiki wa muziki nchini na duniani kwa ujumla. Bayo the Great ni msanii wa kizazi kipya aliyewahi kuvuma na wimbo wa hiphop uitwao Jina Kapuni: https://www.youtube. com/watch?v=qncTaBUAL7E Baada ya ngoma hii Bayo alikaa kimya akifanya shule na baadae kuajiriwa na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na kazi za kijamii kama Solar Aid, The Nature Conservancy, International Citizen Service na Voluntary Service Overseas (VSO) ambako Bayo ameajiriwa mpaka sasa kama Meneja mradi huko Zanzibar. "Kitimtim" ni wimbo wa mduara wenye vionjo vya ragga uliotayarishwa na producer Mesen Selekta toka studio za De Fatality Dar Es Salaam, video ya Kitimtim ambayo ina comedy story ndani yake imetayarishwa na kampuni ya Focus Films chini ya Nick Dizzo. Unaweza kumsapoti Bayo kwa kutazama hapa chini na kushare wimbo huu na wengine....