Skip to main content

Posts

Showing posts from March 8, 2016

MAGAZETINI LEO JUMATANO

JE WAJUA TIMU YA TOTO AFRICANS YA JIJINI MWANZA NDIYO TIMU MASKINI KULIKO ZOTE LIGI KUU NCHINI?

Kocha wa Timu ya Soka ya Toto Africas ya Jijini Mwanza inayoshiriki Liku Kuu nchini, John Tegete (Wa pili kulia) akiwa na "Wananzengo" kutoka Jijini Mwanza ambao wanatarajiwa kuwa wadau wapya wa timu hiyo. Na:George Binagi-GB Pazzo Kwa Mjibu wa Tegete, Toto Africans ndiyo timu Maskini kuliko zote zinazocheza Liku Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Bajeti yake kwa Mwaka ni zaidi ya Shilingi Milioni 495 lakini mapato yake kwa mwaka ni takribani shilingi Milioni 180.  Inakadiriwa kuwa hakuna timu nyingine yenye matapo ya chini kama hayo miongoni mwanza timu za Liku Kuu Tanzania Bara hivyo kwa hali hiyo Toto Africans inapitia wakati mgumu katika kujiendesha kuliko inavyofikiriwa. Pamoja na ugumu huyo, Toto Africans iko nafasi ya Tisa kati ya Timu 16 zinazoshiriki Ligu hivyo hivyo kwa mazingira inayopitia inastahili kuitwa timu bora ambayo haipaswi kutelekezwa na wadau wa soka Jijini Mwanza wakiwemo Wananzengo ambao wameonyesha nia ya kushirikiana na timu hiyo.

MSAADA KWA NDUGU YETU AHMED ALBAITY UNAHITAJIKA (VIDEO)

div class="contents"> Ukiwa ndugu, jamaa na rafiki, bado mchango wako wa hali na mali unahitajika kwa ajili ya ndugu na mpendwa wetu, Ahmed Albaity (pichani) ilikuweza kuendelea na hali yake ya matibabu. Waweza kuhabarika zaidi kupitia taarifa hii ya video hapa chini. Karibuni sana.

UNDP WAFANYA KONGAMANO LA VIJANA, LENGO NI KUWASAIDIA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI

Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Awa Dabo akitoa neno la ufunguzi katika kongamano la vijana na maendeleo, kongamano lililofanyika katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ) Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limefanya kongamano la vijana na maendeleo kujadili jinsi vijana wanavyoweza kutumika kusaidia kuleta maendeleo nchini na kubadili mfumo wa vijana katika kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Akizungumzia kongamano hilo limelofanyika siku ambayo UNDP imetiza miaka 50 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP nchini, Amon Manyama alisema kuwa vijana wana nafasi kubwa katika jamii na kama wakitumika vizuri wanaweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo na hivyo kupitia kongamano hilo wanataraji kuwapa mbinu mpya. Alisema mbali ya kuangala jinsi wanavyoweza kusaidia kupatikana kwa maendeleo pia wanajadili kwa pamoja ili kuona jinsi gani wanaw...

SERIKALI YAZISHAURI TAASISI ZA KIBENKI NCHINI KUWA NA VILABU VYA MICHEZO NA MASHINDANO

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezishauri Taasisi za Kibenki zilizopo nchini kuanzisha timu na vilabu vya michezo ili kukuza michezo pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana walio wengi ambao wana vipaji lakini hawana timu za kuwaendeleza. Hayo yamebainishwa kupitia kwa Waziri mwenye dhamana, Mh. Nape Nnauye mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo tuzo za wachezaji bora walioshinda katika michezo maalum ya BRAZUKA KIBENKI iliyoandaliwa na benki ya Barclays na wadau wengine. Waziri Nape amebainisha kuwa, Nia ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inakuza michezo na kuwa na fursa za kiuchumi kupitia michezo hivyo taasisi hizo zinazo fursa ya kuongeza ajira na ustawi mzuri wa michezo endapo zitaanzisha timu za michezo na kimashindano kwani zinaweza na zinao wajibu huo. Kwa mujibu wa Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya alieleza kuwa, jumla ya timu 16 zilishiriki huku ikianza 28 Novemba...