Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema ushiriki wa baba katika malezi na makuzi ya watoto ni muhimu katika kujenga kizazi chenye maadili mema na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa, hatua inayosaidia kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2050. RC James alitoa kauli hiyo wakati akifungua mdahalo wa pamoja wa kujadili ajenda ya malezi uliofanyika katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (MUCE) mkoani Iringa, aliyoandaliwa na taasisi ya Montessori Community of Tanzania (MCT) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kupitia Idara ya Ustawi wa jamii mkoa. Alisema baba ana nafasi kubwa katika malezi ya watoto na kwamba ushiriki wake husaidia watoto kukua katika mazingira ya upendo, ulinzi na maadili mema, hali inayochangia kujenga jamii imara na yenye uwajibikaji. “Malezi bora ya mtoto hayawezi kufanywa na mzazi mmoja pekee. Ushirikiano wa baba na mama ni muhimu ili mtoto akue katika mazingira yanayomjengea nidhamu, maadili na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa,” alisema RC James. ...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.