Skip to main content

Posts

Showing posts from May 4, 2011

MAFISADI WATESA KWA ZAMU!

Na Gustav Chahe, Iringa Jumla ya watuhumiwa wanane (8) ambao walitakiwa kupelekwa mahakamani kwa sababu za ubadhilifu wa pesa za mradi wa kijiji cha Madege umeingia dosari na wanakijiji kuutupia uongozi lawama za kushindwa kufanya hivyo. Zaidi ya shilingi milioni ishirini na moja (21m/-) za mradi huo ambao unaendeshwa kwa ufadhili wa Districts Agricultural Development Programme Support (DADS), yaani mpango wa kilimo wilayani, kutoka Denmark ulitiwa dosari na baadhi ya wanakijiji walioamua kujinyakulia fedha kinyemela na kuzitia mifukoni mwao. Kijiji hicho kilipata bahati ya ufadhili wa mashine mbili zenye vinu vya kukoboa na kusaga kwa ajili ya maendeleo ya kijiji hicho licha ya kuwa kinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kila aina ambazo zinahitaji nguvu kubwa itumike ili kujikwamua nazo. Hasara hiyo inatokana na usimamizi mbovu wa wale waliopewa dhamana na kijiji kusimamia ikiwa ni pamoja na kutokuwa na na mwongozo wa uendeshaji na kuzitumia mashine hizo kama mali zao binafs...