Skip to main content

Posts

Showing posts from December 3, 2010

MBEGA ANG'OWA MAPAZIA NA SAMANI OFISI YA MBUNGE

Tumaini Msowoya, Iringa VITENDO vya wabunge wa CCM kuhamisha samani na vitu vingine kwenye ofisi za wabunge majimboni, jana liliibukia Iringa Mjini ambako mbunge mpya kwa tiketi ya Chadema, Peter Msigwa amedai kuikuta ofisi ikiwa imeondolewa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kung'olewa kwa mapazia. Msigwa anadai kuwa vitu hivyo vimeondolewa na mbunge aliyemaliza muda wake, Monica Mbega, ambaye alianguka vibaya kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuliongoza jimbo hilo kwa miaka kumi. Kitendo hicho kimeibuliwa siku chache baada ya taarifa za kuondolewa thamani na vitasa kwenye ofisi ya mbunge wa Jimbo la Nyamagana. Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha ndiye aliyeng'oa samani hizo baada ya kushindwa na mgombea wa Chadema, Ezekiel Wenje. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jana, Msigwa ambaye alianza kazi Jumatatu, alidai aliikuta ofisi hiyo ikiwa katika hali ya uchafu huku ikiwa haina mapazia, kompyuta, simu, nyaraka wala faili za kuhifadhia taarifa muhi...