Skip to main content

Posts

Showing posts from March 7, 2026

DC Sitta Apongeza Mikopo Ya Wanawake Manispaa Ya Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamini Sitta , ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa jitihada zake za kutoa mikopo kwa wanawake, akisema hatua hiyo imekuwa chachu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za maendeleo. Sitta alitoa pongezi hizo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wanawake yaliyofanyika katika Manispaa ya Iringa, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani kinachoadhimishwa Machi 8 kila mwaka. Kimkoa wa inafanyikia Mji Mafinga. Alisema mikopo inayotolewa kupitia halmashauri imewasaidia wanawake wengi kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi, jambo linalochangia kuboresha maisha ya familia na jamii kwa ujumla. Aidha, aliwataka wanawake kutumia vizuri fursa za mikopo wanazopewa ili kujenga uchumi imara na kuleta maendeleo endelevu katika jamii. Kwa upande wake, Mkurugenzi  wa Manispaa ya Iringa Zaina Mlawa ulieleza kuwa utaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanaw...

VIWANDA MKOANI PWANI VYATAKIWA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI

  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akizungumza na menejimenti ya Kiwanda cha Keds Tanzania Co. Ltd kinachozalisha bidhaa mbalimbali za usafi katika ziara ya kikazi Mkoani Pwani. Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, akitembelea maeneo mbalimbali katika Kiwanda cha Aluminium Trailers Ltd wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya Wilayani Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026. Alioambatana nao ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Mkurugenziwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma na Watendaji wenginekatika Ofisi ya Waziri Mkuu. Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda na Watendaji wengine katika Ofisi yaWaziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) wakifuatilia maelekezo ya Naibu Waziri waNchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo (hayupopichani), wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya katika Wilaya Kibaha Mkoani Pwani Machi 2-3, 2026. ...