Skip to main content

Posts

Showing posts from July 6, 2015

ZAIDI YA WATU 600 WATOA MAONI JUU YA UTENDAJI KAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

Pichani ni muonekano wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania ndani ya Karume Hall katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar. Pichani ni wananchi wakitembelea banda hilo na kupata taarifa mbalimbali za shughuli za Umoja huo nchini Tanzania.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog ). Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa mwananchi katika picha za viongozi mbalimbali waliowahi kuwa Makatibu wakuu wa Shirika la Umoja Mtaifa duniani ambalo hivi sasa linaongozwa na Ban Ki-Moon. Pichani juu na chini ni Ismael Mnikite (kushoto) kutoka kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ‘Sabasaba’, ndani ya viwanja vya Mwl. J.K Nye...

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA WAMPONGEZA KATIBU WA CCM IRINGA MJINI

katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA MWAMPASHI katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA MWAMPASHI  KEKI ILIYOKUWA IMEANDALIWA SIKU YA SHEREHE HIYO. Baadhi ya wanachama  wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini. NA FREDY MGUNDA, IRINGA Baadhi ya wanachama  wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini wamefanya  mahafari yao katika ukumbi wa chama hicho sabasaba. Wakizungumza wakati wa sherehe hiyo wanafunzi hao wamesema kuwa sas ccm italajia kurudisha jimbo la iringa mjini kwasababu tayari makatibu  wa chama hicho wameweza kuwarudisha vijana kukipenda chama hicho.

IPC WAPATA VIONGOZI WAPYA KWA MIAKA MITATU IJAYO

Msimamizi wa uchaguzi  Hakimu Mwafongo (kushoto) akitangaza matokeo  katika mkutano mkuu wa tatu wa mwaka uliyofanyika Ukumbi wa Lutheran Center mjini Iringa. Kulia ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi, Sofia Mpunga. Mgombea Tukuswiga Mwaisumbe katika nafasi ya katibu akiomba kura Mtia nia Conrad Mpila katika nafasi ya makamu mwenyekiti akiomba kura. Mtia nia Frederick Siwale katika nafasi ya makamu mwenyekiti akiomba kura. Mtia nia Jackson Manga katika nafasi ya makamu mwenyekiti akiomba kura. Mtia nia Francis Godwin katika nafasi ya katibu na makamu mwenyekiti akiomba kura. Na Friday Simbaya, Iringa KLABU ya Waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) imepata viongozi wapya watakaokuwa madarakani kwa miaka mitatu ijayo katika uchaguzi wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jana mjini Iringa. Akitangaza matokeo ya uchaguzi hayo msimamizi wa uchuguzi, Hakimu Mwafongo, akisaidiana na msaidizi wake, Sofia Mpunga alimtan...

SHAMRASHAMRA ZA MANUNUZI YA BIDHAA KATIKA BANDA LA MeTL GROUP MAONYESHO YA SABASABA

Ofisa Mtendaji wa Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack, akisikiliza maoni kutoka kwa mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la Kampuni ya MO Assurance lililopo ndani ya banda la MeTL Group katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kutimua vumbi kwenye viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO, (MO ASSURANCE), Ravinshankar Venkatrama (kulia) akifurahi jambo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji alipotembelea banda la MO Assurance kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea kutimu vumbi jijini Dar. Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group, Hussein Dewji, akipata maelezo kutoka kwa kijana anayetoa huduma kwenye bidhaa za Sundries zinazotengenezwa na kampuni ya MeTL Group. Kulia ni msimamizi wa duka la bidhaa za Sundries, Sandeep Gaur alipotembelea maonyesho ya Sabasaba.

MODEWJIBLOG YANG’ARA MAONYESHO YA SABASABA HUKU IKITIMIZA MIAKA 7

Pichani juu na chini ni Meneja Mwendeshaji wa tovuti ya Modewjiblog, Zainul Mzige akiwapa ufafanuzi wadau waliotembelea banda la tovuti hiyo lililopo MeTL Pavillion katika maonyesho ya kimataifa ya kibiashara ya Sabasaba yanayoendelea katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Bw. Zainul pia ametumia fursa hiyo kutaja umri wa tovuti hiyo ambapo amesema sasa inatimiza miaka saba(7) tangu ilipoanzishwa na kuwa inatarajia kuadhimisha “birthday”itakapofika mwezi wa tisa mwaka huu na amewataarifu wadau kukaa mkao kujiachia.  Na Modewjiblog team Tovuti mahiri ya habari ya modewjiblog leo imevuta umati wa watu wanaotembelea maonyesho ya 39 ya kimataifa ya kibiashara Sabasaba katika banda lake lililopo MeTL Pavillion. Wengi kati ya watu hao walikusanyika kutaka kujua ni jinsi gani tovuti inavyofanyakazi kwa haraka na usahihi sambamba na picha za matukio yanayokuwa yamejiri kwenye habari husika. Akitoa maelezo kwa kina ...