Skip to main content

Posts

Showing posts from May 24, 2018

TANZANIA BADO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam, juu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka. WAKATI tukielekea katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani, Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ambapo asilimia 61 ya nchi inakabiliwa na jangwa. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho hayo ambayo huadhimishwa Juni 5 kila mwaka. “Tukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya Manzingira Duniani, hali ya uhifadhi wa mazingira nchini inachangamato kubwa, asilimia 61 ya nchi yetu inakabiliwa na jangwa,” amesema Makmaba. Amesema sababu ya hali hiyo nikutokana na kilimo, ufugaji na uvuvu usioendelevu ambao umepelekea upotevu wa viumbe hai, kuaha...