Skip to main content

Posts

Showing posts from May 9, 2016

UVUNJAJI WA SHERIA

Pamoja kwamba kuna kibao kinachokataza kutofanya  shughuli zozote zile katika ofisi ya maliasili na utalii,  wananchi hao walikutwa wakutenganeza gari eneo hilo bila kujali ilani ya kibao kama mpigapicha wetu alivyowakuta wakifanya shughuli katika Mtaa ya Ujasili (Ujasili Road) Mlangege Gereji Manisapaa ya Iringa, mkoani Iringa.

AZANIA BENKI YASHEREHEKEA SIKU YA MAMA KWA KUGAWA DAWA NA VIFAA VYA USAFI HOSPITALI YA AMANA

Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kulia), kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa benki hiyo, akimkabidhi kiongozi wa wagonjwa wa ndani wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Francis Yango (kushoto), dawa na vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh.milioni 5 vilivyotolewa na benki hiyo ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake Dar es Salaam leo asubuhi. Wapili kulia ni Muuguzi wa zamu,Getrude Massawe na Antusa Lasway. Wafanyakazi wa benki ya Azania wakiwa mbele ya vifaa na dawa walivyotoa msaada kwa Hospitali hiyo. Hapa ni furaha tupu kabla ya kukabidhi msaada huo. Mwonekano wa maboksi yenye msaada huo baada ya kupokelewa. Vifaa hivyo vikipelekwa kwa walengwa. Mkurugenzi wa Mikakati na Biashara wa Benki ya Azania, Mwanahiba Mzee (kushoto), akimkabidhi dawa za meno na sabuni, Judith Kimei katika wodi ya wazazi. Kulia ni Muuguzi wa zamu Antusa Lasway. Ofisa wa benki hiyo, Neema Tumsifu akimjulia hali mtoto aliyezaliwa katika wodi hiy...

HATIMAYE CHAMA CHA ADC CHAFANYA MKUTANO MKUU,MSAJILI AWAMWAGIA PONGEZI

Waziri wa kilimo wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar amnbaye ni mlezi wa chama cha ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE -ADC nchini Tanzania Mh HAMAD RASHID akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho unaofanyika Jijini Dar es salaam leo(Picha na EXAUD MTEI) Baada ya chama cha ALIANCE FOR DEMOCTARIC CHANGE –ADC kuingia katika migogoro ya kiuongozi ndani ya chama hicho siku za hivi karibuni Hatimaye hali ya Amani imerejea ambapo chama hicho leo kimeingia katika mkutano mkuu uliowakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka kila kona ya nchi. Katika mkutano ambao umehudhuriwa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwemo waziri wa kilimo wa serikali ya Zanzibar ambaye alikuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho ambaye pia ndiye mlezi wa chama Mh HAMAD Rashid,viongozi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho. Makamu mwenyekiti wa ADC Mama ADELA STOLIC akihutubia wakati akifungua mkutano huo Mkuu mapema leo Akizngumza wak...

TIGO YASHIRIKIANA NA MADEREVA WA BODABODA UKEREWE

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti,akihutubia madereva bodaboda wa wilaya yake jana wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa madereva hao na mtandao wa Tigo kwa ajili ya utendaji wao wa kutoa huduma ya usafiri ,Wa pili toka kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya ziwa, Ali Maswanya na Mkurugenzi wa Mikakati wa Tigo Kobbina Awuah(kulia) Mkurugenzi wa Kanda ya ziwa wa mtandao wa Tigo Ali Maswanya, akizungumza wakati wa kuzindua ushirikiano wao na madereva Bodaboda Wilaya ya Ukerewe jana, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Joseph Mkirikiti na Mkurugenzi wa Mikakati wa Tigo Kobbina Awuah(kulia) Madereva Bodaboda Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza,wakinyoosha mikono juu kuashilia kuzinduliwa kwa umoja wao na Mtandao wa Tigo,kwenye hafla iliyofanyika  Baadhi ya bodaboda zikiwa nje ya eneo hilo la ukumbi wa Mmikutano Ukewe. Share on Facebook Share on Twitter