Makamu wa Shule ya Sekondari Pomerini wilayani kilolo, mkoani Iringa Allan Emmanuel Ngede ameanika siri ya kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, kwamba ni kutokana na sapoti ya wazazi, walimu, serikali ya kijiji na serikali kwa ujumla pamoja na wadau. “Siri ya mafanikio ni umoja wetu kati ya wazazi, walimu, wanafunzi, serikali ya kijiji pamoja serikali kuu kwa kuweka viwango vinavyotakiwa katika kuboresha elimu nchini…,” alisisitiza makamuwa shule huyo. Alisema kuwa shule ya Pomerini imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika ya shule 20 ambapo wanafunzi 53 wote wamefaulu na kupata sifa za kujiunga na vyuo, isipokuwa mwanafunzi mmoja tu ambaye amekosa sifa ya kujiunga na chuo kutokana na matatizo ya kinidhamu. Ngede akiongea na Nipashe jana alisema kuwa wanafunzi wengi walifanya vizuri katika masomo ya history na kiingereza kuliko masomo ya jografia na Kiswahili. Alisema kuwa katika matokeo hayo wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi si...
Pamlomo-Sauti Ya Jamii (SYJ) is essentially a digital news platform that shares different types of news updates — social, political, economic, sports, entertainment, and community stories. From the context you’ve given, it is based in Iringa, Tanzania, and functions mainly as an online outlet (likely through social media such as Facebook, YouTube, or other channels) where audiences can get real-time updates.