Skip to main content

Posts

Showing posts from July 9, 2018

Taasisi ya Mo Dewji yatoa Milioni 125 kugharamia matibabu ya watoto wenye saratani

Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula akikabidhi mfano wa hundi ya Tsh. 125 Milioni kwa wawakilishi wa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Fedha hizo zitatumika kugharamia matibabu ya watoto wenye saratani. Na Mwandishi Wetu Taasisi ya Mo Dewji imetoa msaada wa Tsh. 125 Milioni kwa kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ili kusaida kugharamia matibabu ya magonjwa ya saratani kwa watoto wanaopatiwa huduma katika kituo hicho. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Meneja Miradi wa Taasisi ya Mo Dewji, Rachel Chengula alisema msaada huo ni mwendelezo wa misaada ambayo imekuwa ikitolewa na taasisi kwa kituo hicho. Alisema wanatambua hali ngumu ambayo wanapitia watoto hao wanapouguza magonjwa ya saratani, hivyo wanaamini msaada huo utasaidia kuboresha huduma kwa watoto waliopo kituoni hapo na k...