Skip to main content

Posts

Showing posts from April 14, 2015

SERIKALI YASEMA UJENZI WA KITUO CHA MAFUTA NDIUKA NI SALAMA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (mbele kulia) akitoa taarifa ya mkoa wa iringa ya mafanikio ya utekelezaji wa matokeo makubwa sasa (BRN) Julai, 2013 hadi kufikia Februari, 2015 wakati mkutano na waandishi wa habari jana.  Serikali ya Mkoa wa Iringa imewatoa hofu wananchi kuhusu ujenzi wa kituo cha mafuta kinachojengwa eneo oevu (wetland) ya Mto Ruaha eneo la Ndiuka Ipogolo, Manispaa ya Iringa.  Akitoa taarifa ya Mkoa wa Iringa ya mafanikio ya utekelezaji wa matokeo makubwa sasa (BRN) Julai, 2013 hadi kufikia Februari, 2015, kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho hautakuwa na adhari zozote za kimazingira. Alisema kuwa uongozi wa mkoa ulipata taarifa kuwa ujenzi wa kituo cha mafuta (petrol station) ulikuwa unatarajiwa kuanza katika Kiwanja Namba 30/1 Kitalu “A” kilichopo eneo la Ndiuka Ipogolo katika Manispaa ya Iringa.  Aidha, alisema kuwa ujenzi huo ulikwisha pata kibal...

MAGAZETI YA LEO APRIL 14