Skip to main content

Posts

Showing posts from February 25, 2014

SHULE YA PERAMIHO GIRLS YAONGOZA KIMKOA MATOKEO KIDATO CHA NNE

Na Friday Simbaya, Songea Wakati Shule ya St. Francis Girls ya Mbeya ikishika nafasi ya kwanza kitaifa, nayo Shule ya Peramiho Girls ya Ruvuma imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa pia katika matokeo ya kidato cha nne 2013, imefahamika. Katika uchunguzi waliofanya na MWANDISHI WA MWENGE, ulimebaini kuwa Shule ya Wasichana Peramiho ya wilayani Songea vijijini, mkoani Ruvuma imeshika nafasi ya kwanza kimkoa kati jumla ya shule 113 na kushika nafasi 21 kitaifa kati jumla ya 3256 nchini. Akizungumza na Mkuu wa Shule, Bi. Lucida Msabila alisema kwamba alikuwa na uhakika wa shule yake kufanya vizuri kutoka na maandalizi mazuri waliopata wanafunzi wa shule hiyo katika masomo. Akielezea siri ya mafankio hayo Msabila alisema shule yake ilifanya vizuri kutokana ushirikiano mzuri ulipo kati ya wanafunzi, walimu na wazazi, ambapo mwaka 2012 lifanikiwa   kushika nafasi ya pili kimkoa. “Siri ya mafanikio nikujipanga tu kutoka mwanzo pamoja na kuwa na mpango kazi kwa...