Skip to main content

Posts

Showing posts from November 10, 2017

SERIKALI YATOA AGIZO KWA WAKUU WA VYUO VIKUU KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI

Serikali imewaagiza wakuu wote wa vyuo vya elimu ya juu kuacha urasimu katika utoaji wa fedha kwa wanufaika wa mikopo ambao wana makubaliano na Serikali. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema leo bungeni ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Spika Job Ndugai lililotaka serikali kutoa kauli kuhusu wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutakiwa kutoa fedha ili wasajiliwe kabla ya kupata mikopo. Agizo la Spika lilitokana na Mwongozo uliombwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Martha Mlata ambaye alieleza bunge kuwa wanafunzi wamekuwa wakihangaika vyuoni baada ya kutakiwa walipe fedha za usajili kabla ya kupewa mkopo. "Serikali imeshawaagiza wakuu wa vyuo vya elimu ya juu kuacha urasimu katika utoaji wa fedha kwa wanufaika kwa mikopo ambao wana makubaliano na Serikali," amesema. Amesema inasikitisha sana kuona baadhi ya vyuo vinadiriki hata kuwakataa wanafunzi waliowadahili wao wenyewe au vinawalazimisha wachukue programu tofauti...

MIMBA ZA UTOTONI KUPUNGUA,SERIKALI YASHIRIKIANA NA MASHIRIKA BINAFSI KUTOA ELIMU,

Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) Koshuma Mtengeti, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam SERIKALI imejipanga kupunguza mimba za utotoni kwa asilimia 27 kwa kipindi cha miaka mitano kinachoanzia 2017 hadi 2022 lengo likiwa ni kuhakikisha mototo wa kike anapata haki yake ya elimu. Hayo yamesema leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maendeleo ya watoto kutoka Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai wakati wa Kongamano la Mtoto wa Kike , liloandaliwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto wa Kike (CDF) kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo Uswidi ( Swedish International Development Cooperative Agency-SIDA). Mussai amesema kwa sasa serikali imeandaa mpango kazi wa Taifa wa kotokomeza ukatili wa kijinsi kwa upande Mimba za Utoto. “Katika Mpango huu tumeanza kupunguza mimba kwa asilimia 27 kwa watoto na tunaamini mpango huu utasaidia kundokana na tatizo hili”amesema Amesema katika ...

SOMA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NA TUMBUSI BLOG

MAAZIMISHO YA AROBAINI YA IMAM HUSSEIN : SHEIKH JALALA ATAKA WAISLAMU KUENZI MAFUNDISHO YAKE

Ikiwa bado siku moja kukamilika kwa siku ya arobaini tokea kujitoa muhanga kwake Imam Hussein ambaye pia ni Mjukuu wa Bwana Mtume Muhammad ( S.AW ), Watanzania wametakiwa kuenzi mafundisho yake kwani enzi za uhai wake Imam alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa utukufu wa mwadamu, heshima yake unaenziwa kwa kiasi kikubwa na pia hakuna ubaguzi wa aina yoyote unao endekezwa. Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Kiongozi Mkuu wa Waislam Dhehebu la Shia Ithnasheriya Tanzania Sheikh Hemed Jalala amesema Waislamu takribani Milioni 30 watakwenda katika kaburi la Mjukuu huyo wa mtume kuazimisha siku hiyo huku wakikumbuka mafunzo yake matakatifu ya kumtukuza Mwanadamu na kupinga kabisa aina yeyote ya ukandamizaji na unyanyapaa kushamiri miongoni mwa Wanadamu. “Imam Hussein alikuwa ni mtu aliyependa kuenzi utakatifu, utukufu na kuheshimu utu wa Mwanadamu…darsa zake zote ukizisoma utaona alikuwa akisisitiza kuhusu watu kushirikiana, hakupenda kabisa watu kunyanyap...

WAZAZI WAASWA KUWASOMESHA WATOTO WA KIKE

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Spring Valley iliyoko katika manispaa ya Iringa wakiwa katika mafunzo ya vitendo shuleni hapo. NA DENIS MLOWE, IRINGA WAZAZI na Walezi wameaswa kuwasomesha watoto wa kike na kuachana na fikra potofu kuwa kumsomesha mtoto wa kike ni kupoteza rasilimali fedha kwani maisha ya sasa bila elimu ni changamoto kubwa kwa mtoto wa kike. Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Kenneth Komba kutoka Idara ya Elimu mkoa wa Iringa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Spring Valley iliyopo Mkoani Iringa. Alisema kuwa mtoto wa kike akipatiwa elimu kuna uwezekano mkubwa kwa taifa kuwa na maendeleo kutokana na kuwajibika kwao katika maisha ya kila siku hivyo wazazi na walezi ni muhimu kuwasomesha watoto wa kike kwa lengo la kuendeleza ndoto walizonazo. Alisema kuwa jukumu la kusomes...

ROAD SAFETY EDUCATION A KEY FACTOR TO REDUCE ROAD TRAFFIC ACCIDENTS

SOME road accidents in the developing countries like Tanzania are caused by several factors including superstition belief for sacrifices for economic interest or benefit and also carelessness. Some of accidents are caused voluntarily by individuals for example when the driver is drank he/she knock a person and pass away, and other road accidents caused involuntarily not a human error, for instance, driver has beaten a horn many times around a corner and he knocks person and die. So in achieving the reduction of accidents, Chegamila Investment being the authorized Toyota dealer based in Iringa town, Iringa Region has organized a ‘Toyota customer’s week’ for them to take their cars for free initial checkup, the Guardian can disclose. Chegamila Investment Manager, Seif Rashid told the Guardian reporter in an interview yesterday that the occasion will take place at Chegamila compounds on 13-18/11/2017. He has asked Iringa residents and its surrounding areas t...