Skip to main content

Posts

Showing posts from January 8, 2013

ELIMU

Wanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Peramiho 'A' wilayani Songea, Mkoa wa Ruvuma wakiwa katika darasa lao na Mwalimu Katona wakiimba wimbo wa shule ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza kwa muhula mwaka 2013.

WANACHAMA 150 WA CCM PERAMIHO WATIMKIA CHADEMA

Na Friday Simbaya, Songea Jumla ya wanachama 150 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), vijana kwa wazee wa Kata ya Peramiho wamekata shauri na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kati yao 130 wamerudisha kadi za CCM na wengine 20 ni wanachama wapya, wakati wa mkutano wa hadhara  uliofanyika eneo la Namihoro sokoni, Wilaya ya Songea (V) mkoani Ruvuma juzi. Kada na mpigadebe wa CCM maarufu, Margret Ndomba (kushoto) akipeana  mkono na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa (NEC CHADEMA), Edson Mbogolo baada  aliyakurudisha kadi tatu za CCM, yaani kadi ya UVCCM, kadi ya UWT na CCM  wakati wa mkutano wa hadahra wa chama hicho uliyofanyika Namihoro  katika Kata ya Peramiho Wilaya Songea, Mkoani Ruvuma juzi. Miongoni mwa wanachama waliorudisha kadi za CCM na kuamua kujiunga na Chadema ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM wa Tawi la Peramiho, Bruno Mwitumba pamoja na kada wa CCM Margret Ndomba aliyerudisha kadi tatu; kadi ya UVCCM, kadi ya UWT na CCM. A...