Skip to main content

Posts

Showing posts from February 3, 2014

MASHINDANO YA KOMBE LA ANSGARI (ANSGAR CUP) MWAKA 2014 YANUKIA

Dkt Ansgar Mashindano ya Kombe la Ansgar (Ansgar Cup) tarafa ya Ruvuma, wilayani Songea vijijiin, mkoani Ruvuma yanatarajia kutimua vumbi katika viwanja vya Ansgari vilivyopo Peramiho kuanzia tarehe 13/04/2014 na kumalizika 22/06/2014 Siku ya Ekaristi Takatifu, imefahamika. Akitangaza ratiba hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Mfadhili, Dkt. Magnus Mwanyika wakati kikao cha maandalizi ya mashinadano hayo kulichofanyika jana eneo la Mgahawa wa Peramiho, alisema kuwa mashindano hayo yataanza tarehe 13/04/2014 ngazi ya kata na fainali ngazi ya tarafa yatafanyika siku ya Ekaristi Takatifiu tarehe 22/06/2014. Dkt. Mwanyika aliwaambia wajumbe kamati ya maandalizi kuwa mwaka kutakuwa na mabadilko kidogo kwa upande wa zawadi , ambapo alifafanua kuwa mshindi wa kwanza atapata zawadi ya 300,000/- (futiboli na netiboli), wa pili ataondoka na shilingi 250,000/- na mshindi wa tatu atajipatia 150,000/- (mpira wa miguu na pete) ukilinganisha na mwaka jana. “Zawadi mwak huu z...