Skip to main content

Posts

Showing posts from March 14, 2011

JAMBO LA MSINGI NI KUELEZA UKWELI, ILI KUPATA HALI HALISI...

Na Friday Simbaya, Songea MKOA wa Ruvuma hivi karibuni walikuwa na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Kutathmini maendeleo ya elimu mkoani mwaka 2011, uliyofanyika hapa Peramiho katika Halmashauri ya Songea. Mkutano huu ulilenga kutathmini utekelezaji wa kazi na kupima ufanisi wa shughuli za maendeleo ya elimu mkoani hapa. Aidhi, kuanzia mwaka 2008 kumekuwepo pia mikutano ya wadau ya kutathmini maendeleo ya elimu ngazi ya wilaya/ halmashauri, kata na shule; ambao hufanyika kabla ya kikao cha tathmini ya kimkoa. Akifungua mkutano huo mkuu wa wadu wa elimu wa kutathmini maendeleo ya elimu, mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Christine Ishengoma aliwaambia wadau kwamba jambo la msingi ni kueleza ukweli, ili kupata hali halisi ya utekelezaji wa vitendo uliyofanyika, na sio taarifa za maandishi au maneno tu, tofauti na uhalisia. Alisema kuwa lengo hasa la kufanya tathmini katika ngazi zote hizo ni kupima utekelezaji wa mipango na malengo waliyojiwekea kwa kipindi kilichopita; kwa kuzingitia eneo...