Skip to main content

Posts

Showing posts from February 27, 2018

RC Masenza Awataka Wakandarasi Kufanya Kazi Kwa Ufanisi Na Viwango Vya Ubora

Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Iringa Iringa Eng Juma Wambura (wa pili kulia) akimkabidhi mmoja wakandarasi mkataba (Picha na Friday Simbaya) IRINGA: Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka wakandarasi wote walioshinda zabuni kufanya kazi kwa kuzingatia muda uliopangwa na viwango vya ubora wa kazi.  Alisema kuwa Serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayefanya kazi chini ya muda uliopangwa kwenye Mkataba, Lakini pia haitamvumilia Mkandarasi atakayefanya kazi chini ya viwango.  RC Masenza alisema hayo jana wakati akishuhudia hafla fupi ya kutiliana saini mikataba ya miradi ya ujenzi wa barabara kati ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Iringa na wakandarasi walioshinda zabuni kwa mwaka wa fedha 2017/2018.  Alisema kuwa katika kuhakikisha ufanisi wa kazi na ubora unaotakiwa, Serikali imeajiri Mameneja wa TARURA katika kila halmashauri.  “Ju...