TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho kitaweza kufanya kazi. "Kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na...