Skip to main content

Posts

Showing posts from August 4, 2011

WAHABESHI WAGOMA KULA TENA LUDEWA

MAHABUSU 87 kutoka Ethiopia wanaoshikiliwa na Idara ya Uhamiaji katika Gereza la Ibihi lililoko nje kidogo ya mji wa Ludewa wamegoma tena kula siku ya nne sasa huku wengine watatu wakitundikiwa madripu ya maji na chakula katika Hospitari ya Wilaya ya Ludewa. Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu wa Magereza (ASP), Babilas Masimo kwa upande wake alikiri kutokea kwa mgomo huo kwa mara ya tatu tena, lakini hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwa kusema kuwa yeye alikwisha kuwajulisha wanaohusika na maamuzi. Mganga Mkuu wa Hospitari ya Wilaya ya Ludewa, Dkt. Happines Ndosi alikiri kuwapokea mahabusu watatu wakiwa wamedhoofu kwa njaa ambapo miongoni mwao mmoja alikutwa na Malaria ingawa siyo ugonjwa uliomfikisha hospitalini hapo. Dkt. Ndosi amelalamikia kitendo cha kuendelea kuwashikilia mahabusu hao kuwa kinawamalizia dawa kwa sababu hawamo kwenye bajeti waliyonayo na kwamba analazimika kuchukua dripu za akin...

DC LUDEWA APUUZA MAAZIMO NA AGIZO LA BARAZA LA MADIWANI

  MKUU wa Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa Bi. Georgina Bundala amepuuza maazimio na agizo la Baraza la Madiwani lililomtaka kuwakutanisha na Kamishna wa Madini Kanda ya Mbeya ili kujua sababu zinazopelekea wachimbaji na watafiti kuvamia maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo bila wananchi kujulishwa na badala yake amemleta kamishna huyo kimyakimya na kuanza kumtembeza na kufanya mikutano ya hadhara kwa badhi ya Kata tu. Katika Baraza Kuu la Madiwani (Fully Council) lililofanyika Ijumaa Julai 15 mwaka huu madiwani waliazimia na kuitaka ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kumwandikia barua kamishina wa madini kanda ya Mbeya kufika Ludewa na kukutana kwanza na madiwani hao ili kujua nini kinaendelea wilayani mwao, sheria za madini zinasemaje kuhusu stahili na haki za mwananchi kwa watafiti na wachimbaji madini. Katika Baraza hilo la madiwani Bi. Georgina Bundala alikuwa mgeni rasmi na baada ya kufungua ...

IPC wapata viongozi wapya

Na Friday Simbaya, Iringa. HAKUNA haja ya kuendekeza makundi kwa lengo la kuibomoa chama ambacho msingi wake ni umoja, mshikamano na kuinuana kwa waandishi. Hayo yalisemwa na aliyemaliza muda wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa (IPC ), Keneth Simbaya wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani hapa. Simbaya alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wananchama kuamua kuunda kundi lao kwa kudanganyana wengine na kusababisha baadhi ya wanachama  na kuwasihi wanachama kujenga imani ndogo ndani ya chama na kusababisha wengine kuamua kutojiunga na chama. Alisema kuwa hakuna mtu aliye bora kuliko mwingine ni lazima kila mwananchma kujishusha na kukubaliana kwa lengo moja la kuwasaidia walio chini ili wafike wanapostahili kwa kuwapatia mafunzo na uzoefu zaidi mbali na elimu aliyoipata shuleni. “Mungu aliumba watu wa aina mbalimbali na aliwapenda sana ...