Skip to main content

Posts

Showing posts from October 28, 2010

HABARI KATIKA PICHA

MAWAKALA mbalimbali wa magazeti waliyoketi mkono wa kushoto wakiwa wanagawa magazeti asubuhi ya leo kwa mavendors kwa ajili ya kuyauuza kwa wateja yao. Magazeti yao huchapishwa jijini Dar es Salaam na kufika hapa mkoani Iringa kati ya saa1:70 na zaidi.  BAADHI ya wakazi wa Mjini Iringa wakiwa wamepanda kwenye mti ilikufuatilia mkutano wa kampeni ya uchagazi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jioni ya leo, ambao ulitarajiwa kuhutubia na mgombea urasi kupitia chama hicho Dr. Wilbroad Slaa lakini bahati mbaya hukufika kutokana uwezo ulionje ya uwezo wao. MKAZI mmoja wa Iringa Mjini (kushoto) ambayo jina lake halikupatikana mara moja alikutwa akinunua picha ya kuvaa shingoni ya Mgombea Urasi wa CHADEMA Dr. Slaa kutoka kwa mwanachama hicho leo katika mkutano wa kampeni ya uchaguzi uliofanyika viwanja vya Mwembetogwa mjini hapa, zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu oktoba 31, 2010.

VIZIWI HAWAJUI NI CHAMA KIPI CHA KUCHUGUA OCTOBA 31

Na Francis Godwin, Iringa HUKU ikiwa zikiwa zimebaki siku mbili pekee ili watanzania wote waliojiandikasha na wenye sifa ya kupiga kura kushiriki katika zoezi la uchaguzi wa Rais ,wabunge na madiwani zaidi ya watu walemavu wa kusikia (Viziwi) 2000 katika mkoa wa Iringa kushiriki uchaguzi mkuu katika mchezo wa bahati nasibu. Uchunguzi wa kina uliofanywa na mwandishi wa habari hizi ndani ya mkoa wa Iringa umebaini kasoro mbali mbali ambazo zimefanywa na wagombea karibu wote wa vyama vya siasa wakati wa kampeni zao baada ya kushindwa kuweka mpango mzuri wa kuwafikia viziwi na jamii nyingine yenye ulemavu katika kunadi sera zao. Japo kwa upande wa jumuiko la asasi za kiraia Tanzania mkoani kwa mikoa ya Iringa,Mbeya ,Rukwa na Ruvuma zimeweza kwa kiasi chake kuwakutanisha wagombea wa nafasi ya ubunge na makundi mbali mbali ya jamii wakiwemo viziwi ambao hata hivyo wamepata kusikiliza sera za baadhi ya vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chad...