Skip to main content

Posts

Showing posts from June 24, 2017

ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILE KUWEKWA WAKFU KESHO

Askofu Mteule Mchungaji Blastone Tuluwene Gavile (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Himid John Sagga. IBADA ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gavile, inatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 25, 2017 mjini Iringa. Ibada hiyo, ambayo itaambatana na kuingizwa kazini kwa Msaidizi wa Askofu, Mchungaji Himid Sagga, itafanyika ikiandika historia kwenye Dayosisi hiyo ambapo Askofu Mteule Gavile anachukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenberg Moses Mdegela ambaye amestaafu. Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Nayman Chavalla, amesema tukio hilo maalum ni la pili katika historia ya Dayosisi hiyo, kwani Mchungaji Gavile anakuwa ndiye askofu wa pili tangu kuanzishwa kwake. Aidha, katika ibada hiyo Askofu Mteule Blaston Gavile atamuingiza kazini Msaidi wake Mchungaji Himid John Sagga. Awali akielezea jinsi ibada hiyo itakavyokuwa, Chavalla alisema itaanza k...

SUPERFEO YAUA TENA SONGEA

KAMPUNI ya mabasi ya Superfeo inayosafirisha abiria toka jijini Mbeya hadi mjini Songea leo tena imepata ajali katika eneo la Hangagadinda wilayani Songea na kuua mtu mmoja ambaye alikuwa ni kondakta wa basi hilo.  Meneja huduma wa Kampuni hiyo Fransisi Sengo anasema ni siku moja tu imepita baada ya ajali nyingine ya superfeo kutoka Mbeya kuja Songea kupata ajali juzi katika kijiji cha Mbangamawe wilayani Songea na kuua dereva wa basi hilo. Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Songea ambaye ndiye Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ametembelea eneo la ajali ambapo Inadaiwa ajali hiyo ilisababishwa na dereva ambaye alikuwa anaongea na simu huku anaendesha gari.  Mgema ameagiza vyombo vya dola kufuatilia tabia za madereva ikiwa ni pamoja na kuwapima viwango vya ulevi ili kupunguza ajali zisizo za lazima. Mkuu wa wilaya ya Songea pia ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma kuwafariji majeruhi zaidi ya 18 waliolazwa ka...