Skip to main content

Posts

Showing posts from November 30, 2010

JK AWAPASHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAKE KATIKA SEMINA ELEKEZI

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana kwa mara ya kwanza na baraza lake jipya la mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu asubuhi. RAIS Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu, Novemba 29, 2010, amekutana rasmi kwa mara ya kwanza na Baraza la Mawaziri lake jipya pamoja na Naibu Mawaziri na kuwapa maelekezo ya awali ya nini anakitarajia kutoka kwa wateule wake hao. Mawaziri wote 29 na Naibu Mawaziri wote 21 ambao Rais Kikwete aliwaapisha rasmi kushika nyadhifa zao katika sherehe iliyofanyika Jumamosi iliyopita, Novemba 27, 2010, wamehudhuria mkutano huo kwenye Chumba cha Baraza la Mawaziri, Ikulu, Dar es Salaam. Katika mkutano huo uliochukua kiasi cha saa tatu, Rais alianza kwa kuwaeleza mawaziri kuwa katika kipindi hiki cha pili cha uongozi wake hakutakuwepo na muda wa kupoteza, na wala hatakuwa tayari kukubali maelezo ya kwa nini utekelezaji wa majukumu ya msingi umeshindikana. Kwa mara nyingine amewapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri hao akisisitiza: “Mnasta...